2 Samuel 14:23-28

23 aNdipo Yoabu akaenda hadi Geshuri akamrudisha Absalomu Yerusalemu. 24 bLakini mfalme akasema, “Lazima Absalomu aende kwenye nyumba yake mwenyewe; kamwe asiuone uso wangu.” Kwa hiyo Absalomu akaenda kwenye nyumba yake na hakuuona uso wa mfalme.

25 cKatika Israeli yote hakuna mtu yeyote aliyesifiwa kwa uzuri wa sura kama Absalomu. Kuanzia utosi wa kichwa chake hadi wayo wa mguu wake hapakuwa na kasoro. 26 dKila mara aliponyoa nywele za kichwa chake, kwa kuwa alikuwa akinyoa mara kwa mara zilipokuwa zinamwia nzito, alizipima uzito wake ulikuwa shekeli mia mbili kwa kipimo cha kifalme.
Shekeli 200 kwa kipimo cha kifalme ni sawa na kilo 2.3.

27 fWalizaliwa wana watatu na binti mmoja kwa Absalomu. Jina la binti yake aliitwa Tamari, naye akawa mwanamke mzuri wa sura.

28Absalomu akaishi miaka miwili huko Yerusalemu pasipo kuuona uso wa mfalme.
Copyright information for SwhKC